Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa {TAMISEMI} Mhe Josephat Kandege ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa usimamizi mzuri wa fedha za Serikali na kuwataka viongozi wa Halmashauri nyingine kuja kujifunza katika Halmashauri ya Tanga .
Naibu waziri TAMISEMI Mhe Josephat Kandege aliyasema hayo wakati wa ziara yake Mkoani Tanga ambapo alisema Halmashauri ya Jiji la Tanga imeonesha mapinduzi makubwa katika kusimamia fedha za Serikali kwa kujenga jengo la Halmashauri pamoja na dampo.
"Mmeonesha mapinduzi makubwa katika kusimamia fedha za Serikali na mimi nitawambia viongozi mbalimbali waje wajifunze Tanga "Alisema Josephat Kandege
Sambamba na hayo Naibu waziri TAMISEMI Mhe Josephat Kandege alisema kumekuwa na Halmashauri nyingine ambazo zimekuwa haziwezi kufanya maendeleo kama Tanga Jiji walivyoamua kutumia fedha kutoka katika vyanzo vyake vya ndani.
Naibu waziri wa TAMISEMI Mhe Josephat Kandege aliongeza kwa kuwataka viongozi kutoka katika Halmashauri mbalimbali kuona namna gani fedha za ndani zinaweza zikatumika katika kuanzisha miradi mikubwa kama Tanga Jiji ilivyofanya .
Lengo la ziara ya Mhe Naibu waziri wa TAMISEMI katika Jiji la Tanga ni kukagua miradi mbalimbali iliyopo Jijini Tanga ambapo ameweza kutembelea jengo la Halmashauri ya Jiji la Tanga ambalo linaendelea kujengwa pamoja na Dampo .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.