Kuandaa mipango madhubuti ya maendeleo ya upanuzi wa ujenzi wa hospitali, vituo vya afya na zahanati.
Kuandaa mipango ya maendeleo ya upanuzi na ujenzi wa shule za awali na msingi na elimu ya watu wazima kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya 1978 kama ilivyorekebishwa mwaka 1995.
Kupendekeza mipango ya ujenzi au upanuzi wa vituo, viwanja, majengo na mazingira ya burudani, starehe, mapumziko na michezo.
Kuamua juu ya mambo yanayohusu uhifadhi wa mambo ya kale na mandhari mbalimbali yenye sura nzuri.
Kuandaa na kuratibu njia bora juu ya uhifadhi wa nyaraka muhimu kwa ajili ya kumbukumbu hizo zitahifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa Sura ya 288
Kupendekeza njia bora juu ya uhifadhi wa sanaa mbalimbali za ufundi na za maonyesho kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa sura ya 288
Kupendekeza matumizi mazuri ya lugha ya taifa
Kupendekeza namna ya malezi ya vijana ili waweze kuwa wazalishaji katika Taifa
Kusimamia uazishaji wa uendelezaji wa vikundi vya jamii na vya hiari vya wananchi katika Halmashauri kwa mujibu wa Sera wa maendeleo ya jamii
Kusimamia na kuhakiki maeneo ya misitu, mapori na mbuga zilizotengea kama hifadhi ya mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Kupendekeza na kufanya tathmini ya uendelezaji wa mabonde, mito na mabwawa.
Kubuni na kupendekeza namna ya kuthibiti moto
Kubuni na kupendekeza mikakati ya utumiaji wa nishati mbadala, kuzuia ukataji miti ovyo, na kuhimiza upandaji miti kwa wingi.
Kuhakikisha kwamba ukaguzi wa majengo unafanyika mara kwa mara.
Kupendekeza mipango madhubuti ya ujenzi wa barabara vijijini na wilayani kwa ujumla