Wilaya ya inakadiriwa kuwa na Vijana 105,096 (me 48,816 na ke 56,280), kati ya hao wenye ajira rasmi 21,019 (20%), waliojiajiri 47,293 (45%), walio shuleni 18,886 (18%) na wasio na kazi ni 17,898 (17%).
Hatua Zinazoendelea:
Mikopo ya Wanawake na Vijana
Kwa mwaka 2017/18 Halmashauri ya Jiji imetenga Tsh. 671,470,000 kwa ajili ya mikopo ya Vijana na Tsh. 671,470,000 kwa ajili ya wanawake. Halmashauri imewezesha Vijana wa Kikundi cha Mwamko cha Kiomoni pembejeo za kilimo zenye thamani ya Tsh.7,824,500.00 pamoja na kuwawekea miundombinu ya umwagiliaji wa matone. Aidha, Halmashauri iko katika mchakato wa kutoa mikopo ya Jumla ya Tsh.200,000,000/=ambapo Tsh.100,000,000 ni kwa ajili ya Vijana na Tsh.100,000,000/= ni kwa ajili ya wanawake. Pia, uwezeshwaji wa vikundi juu ya uchumi wa viwanda na uandaaji wa maandiko ya miradi umefanyika.
Uwezeshaji wa Wanawake na Vijana
Katika suala zima la uwezeshaji wa vijana na wanawake Halmashauri imetenga viwanja 20 kwa ajili ya wanawake na vijana, ambapo katika viwanja hivyo vitaendelezwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kati 10 vya wanawake na viwanda vya kati 10 (Medium Scale Industries) kwa ajili ya vijana. Aidha katika utekelezaji wa mpango huo makundi hayo yatapewa taratibu maalum za kuchangia kwa ajili ya kujiunga katika makundi hayo ili kuwa mwanachama na kushiriki katika uchumi huo wa viwanda.Utekelezaji wa mpango huu umeanza kwa kukutana na wadau na kuunda kikosi kazi. Tunaamini kuwa mpango huu utawezesha kuwavusha vijana na wanawake kutoka katika wimbi la umaskini.
Uwekezaji wa kiuchumi
Uwekezaji unaotegemewa kuanza katika wilaya ya Tanga ni ule wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda kuja Tanga. Viwanda hususani viwanda vya saruji, kwenye sekta za barabara, reli, bandari, kilimo, ufugaji, biashara utawezesha kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana kwa njia ya kujiajiri au kuajiriwa.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.