Uchimbaji wa Chumvi
Haya ni maeneo yaliyopo kandokando mwa bahari ya Hindi yenye ukubwa wa Hekta 212 yanayofaa kwa uwekezaji wa uzalishaji chumvi. Maeneo haya ni Maere, Chumvini (Kisosora), Mpirani, Ndaoya, Machui, Tongoni, Mwarongo na Chongoleani. Kwa sasa uzalishaji wa chumvi ni tani 6000 kwa mwaka. Chumvi inayozalishwa inatumika kama malighafi kwenye uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani. Kwa kuwa uzalisshaji kwa sasa unafanywa na wazalishaji wadogo wadogo uwekezaji mkubwa unahitajika katika Sekta hii ya chumvi.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.