Uwekezaji katika maeneo ya sekta ya utalii unajumuisha ujenzi wa miundombinu ya kusaidia utalii kama Mahoteli ya kitalii katika fukwe zilizopo Bahari ya Hindi kama vile maeneo ya fukwe za Chongoleani, Mwambani, Tongoni na Mwarongo pamoja na utalii wa kuendesha mashua za mashindano ya baharini na kuogelea kwa kupiga mbizi, vilevile utalii wa utamaduni wa wenyeji wa Tanga na mwenendo wa maisha yao kwa jumla.
Tanga imejaaliwa kuwa na maeneo ya asili ya utalii kama mapango ya Amboni, Magofu ya Tongoni, Kisiwa cha Totten. Kisiwa cha Jambe na eneo la majimoto na majengo ya zamani ya Wajerumani na watu wenye asili ya bara la Asia
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.