Halmashauri ya Jiji yetu imeunganishwa kwa barabara za lami pande zote (Tanga – Muheza, Segera, Korogwe. Tanga – Mkinga, Horohoro (Tanga,Tanzania-Mombasa, Kenya boarder) kasoro barabara ya Pangani-Tanga, ambayo mpango wa ujenzi wake uko kwenye maandalizi.
Halmashauri ya Jiji ina mtandao wa barabara unaokadiriwa kufikia km. 1256.1 asilimia 81.6 % ya hizo yaani km. 1024.6 ndizo zinazohudumiwa na Halmashauri ya Jiji kwa sasa, zilizosalia zinasimamiwa na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).
Mtandao wa barabara
TANROADS
|
Halmashauri ya Halmashauri ya Jiji
|
Jumla
|
||||||
Lami
|
Changarawe
|
Udongo
|
Jumla
|
Lami
|
Changarawe
|
Udongo
|
Jumla
|
|
55.86
|
31.11
|
144.5
|
231.50
|
106.4
|
217.6
|
700.6
|
1024.6
|
1,256.1 |
Mradi Wa Tanzania Strategic Cities Project (TSCP)
Halmashauri ya Jiji la Tanga ni miongoni mwa Miji saba (7) inayotekeleza mradi wa uendelezaji Miji Mkakati (Tanzania Strategic Cities Project – TSCP). Halmashauri kupitia mradi huu imefanikiwa kukamilisha miradi ifuatayo ya miundombinu:
Ujenzi /ukarabati wa barabara za Jiji kufikia kiwango cha lami kilomita 15.3 na taa za barabarani
Ujenzi wa mifereji mikubwa ya maji ya mvua kilomita 5.6 ambayo imewezesha kupunguza tatizo la mafuriko katika Kata za Mabawa, Magaoni na Duga.
Ujenzi wa kituo kipya cha Mabasi na eneo la kuengesha Malori
Ununuzi wa vifaa kwa ajili ya usafi wa mji
Vilevile Halmashauri ya Jiji la Tanga imekamilisha utekelezaji wa miradi ya nyongeza (TSCP – Additional Financing) ya ujenzi wa miundombinu kwa gharama ya Tshs. 9,536,012,640/= ikihusisha:
Ujenzi /ukarabati wa barabara za Jiji kufikia kiwango cha Lami na uwekaji wa taa za barabarani za mfumo wa jua(solar street light) Kilomita 5.03.
Ujenzi wa mifereji midogo ya maji ya mvua Kilomita 3.44 umekamilika katika Kata za Magaoni na Maweni ili kuendeleza jitihada za kuondoa mafuriko kwenye makazi ya wananchi.
Ujenzi wa maabara ya udongo na uwekaji wa vifaa vyake.
Ujenzi wa matenki ya kuhifadhia maji katika stendi ya mabasi na malori
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.