Kitengo cha Teknolojia ya Habari, Mawasiliano (TEHAMA)
Kitengo cha (TEHAMA) kimeanzishwa mwaka 2010 kwa kuunganisha kitengo cha Teknolojia ya Habari Mawasiliano na Mahusiano. Kitengo hiki kina watumishi wa kada mbili, Mafisa TEHAMA na Maafisa Habari
Majukumu ya Kitengo
NA.
|
HUDUMA ZITOLEWAZO
|
JINSI ZINAVYOPATIKANA
|
1
|
Kutoa taarifa za robo au mwaka kwa wananchi na wadau wa maendeleo kuhusu masuala yanayogusa jamii.
|
- Tovuti ya Halmashauri (www.tangacc.go.tz)
- Vipeperushi - Barua pepe - Magazeti, n.k. |
2
|
Kusimamia ufikishwaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi
|
- kampuni za mawasiliano ya simu
|
3
|
Kusaidia jamii kuwa na weledi wa masuala ya mitandao na kuweza kujilinda dhidi ya mashambulizi.
|
- Tovuti ya Halmashauri
- Vipeperushi - Semina na warsha. |
4
|
Kutathimini na kusimamia viashiria vya hatari kuhusiana na miundombinu na mifumo ya TEHAMA
|
- Kuwasiliana na wataalam wa TEHAMA waliopo Halmashauri.
|
5
|
Kutoa miongozo kwa wananchi kuhusu mabadiliko ya njia za utoaji huduma mbalimbali za kielektroniki.
|
- Tovuti ya Halmashauri
- Matangazo - Vipeperushi na semina. |
6
|
Kusimamia mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa fedha na ukusanyaji mapato ya ndani, takwimu, n.k.
|
- Benki
- Mitandao ya Epicor, LGRCiS, BEMIS, HCMIS - Mtandao wa intaneti |
7
|
Kufanya usimikaji na uhuishaji wa programu za kompyuta, na matengenezo ya vifaa vya TEHAMA.
|
- Kufika Kitengo cha TEHAMA
- Kuwasiliana na wataalam wa TEHAMA kwa simu au barua pepe. |
8
|
Kutoa ushauri kuhusu matumizi ya vifaa vya TEHAMA.
|
- Kufika Kitengo cha TEHAMA
- Kuwasiliana na wataalam wa TEHAMA kwa simu au barua pepe. |
Pata Taarifa zinazohusiana na TEHAMA kwa kufuata viunganishi (link) hapa chini
Mwongozo wa Tovuti za Halmashauri
Muongozo wa Matumizi Bora na Salama ya TEHAMA Serikalini - Mwaka 2017
Orodha za namba za simu kwa ofisi zilizo kwenye mfumo wa Mawasiliano wa Serikali (GovNet)
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.