Imeandaliwa na Naetwe Kilango;
Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii ustawi na vijana jijini tanga Bi; Flora Shija Maagi amekemea wanavikundi wababaishaji katika jijini Tanga, ambao hutumia ujanja ujanja katika kuonyesha shughuli za miradi ya vikundi vyao, Hayo yamejitokeza wakati zoezi la uhakiki wa vikundi vinavyotarajiwa kupatiwa mkopo wa Wanawake na vijana linaendelea jijini hapo.
Miongoni mwa kata zilizofikiwa ni pamoja na Msambweni, Mzizima, Kirare, Mabawa, Kiomoni, Chongoleani, Nguvumali, Magaoni, Chumbageni, Ngamiani kaskazini, Duga, Majengo ambapo mkuu huyo wa idara amesema baadhi ya wanavikundi wamekua wababaishaji hasa pale wanapoamua kuonyesha miradi endelevu ya watu binafsi kwa tamaa ya kutaka kukopeshwa kiwango kikubwa cha fedha ambapo wenye miradi hiyo huridhia kwa lengo la kupata fedha hizo kupitia migongo ya wanavikundi hao.
Bi; Shija amesema atasimamia kwa weledi mkubwa zoezi hilo kwa lengo la kuhakikisha fedha hizo zinawafikia walengwa na kwa kuzingatia miongozo, Hata hivyo amesisitiza kwamba suala hilo ni la kisera na pia idara yake inatekeleza ila, Mkuu huyo wa idara amesema mifuko hii si kwaajili ya kuwanufaisha mtu mmoja mmoja ambao tayari walishafanikiwa kuendeleza miradi yao, badala yake wananchi wa hali ya chini wajiunge kwenye vikundi vya kiuchumi na kuanzisha miradi ya viwango vya saizi yao ili kuiendeleza kufikia uchumi wa kati
Akizungumza na maafisa maendeleo walioko chini yake katika ofisi za maendeleo ya jamii jijini hapo Bi; Shija amesema kada hiyo inahitaji nidhamu ya hali ya juu, uwajibikaji na weledi katika kuleta ufanisi. Amewataka maafisa maendeleo ya jamii jijini hapo na hata duniani kote kutoifedhehesha kada kwani ni taaluma pekee mtambuka na yenye wajibu wakuwafanyia wanajamii oparesheni za akili ili kuondokana na mitazamo hasi, fikra potofu halikadhalika kuwawezesha wananchi kutambua fursa zilizopo katika maeneo yao, kuzitumia na kujiendeleza kiuchumi.
Aidha Bi; Shija amesema Halmashauri yake imetenga fedha za kutosha kwaajili ya kuvikopesha vikundi vyote vya vijana na wanawake ambavyo vitakidhi vigezo, pia amewataka wananchi kuzingatia elimu na ushauri wanaopata toka kwa maafisa maendeleo ya jamii katika jiji hilo ili kuweza kufikia viwango vya kukopesheka.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.