Chanzo: Maelezo Blog
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo ametoa agizo kwa Ofisi za Mikoa na Halmashauri zote nchini kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwa vitengo vya Mawasiliano ili viweze kutekeleza majukumu yake.
Mhe. Jafo ametoa agizo hilo Jijini Arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa (AICC) alipokuwa akifunga Kikao Kazi cha 14 cha Maafisa Mawasiliano Serikalini uliohudhuriwa na Maafisa Mawasiliano 300 kutoka katika Taasisi, Idara na Wakala wa Serikali, Mikoa, Majiji, Miji na Halmashauri zote nchini.
“Kuanzia mwaka ujao wa bajeti Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri, Majiji, Manispaa na Miji waweke kipaumbele kwa kutenga fedha za kununua vifaa muhimu kwa ajili ya Maafisa Habari na Mawasiliano ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo,” alisema Mhe. Jafo.
Pamoja na kununuliwa kwa vifaa hivyo, Waziri Jafo pia ameziagiza Halmashauri kuhakikisha maafisa habari wanaingia kwenye vikao vya maamuzi ili wapate na kutoa habari kamili.
“Inawezekana baadhi ya maofisa wa halmashauri wakawa ndio wanawazuia maafisa habari kuingia katika vikao kwa lengo la kuficha baadhi ya taarifa, kuanzia sasa hili jambo sitaki litokee, ni lazima wawe wanaingia kwenye vikao” alisema
Mkutano wa Maafisa Mawasiliano Serikalini unafanyika kila mwaka, ambapo kwa mwaka huu unafanyika kwa mara ya 14. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Chama cha Maafisa Mawasiliano
Video ya Mhe. Waziri Japo alipokuwa akihutubia kwenye kufunga Kikao
Chanzo: Maelezo Blog (blog.maelezo.go.tz)
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.