Viongozi mbalimbali wa serikali hasa ngazi ya Watendaji wameshauriwa kuzingatia umuhimu wa ukusanyaji wa data katika Taasisi mbalimbali ili kuweza kuepuka hasara zinazojitokeza katika ukusanyaji wa data hizo.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Datalab Omary Bakari wakati wa kufunga mafunzo ya jinsi ya ukusanyaji wa data kwa njia ya sayansi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga.
“Leo hii tumekutana na wadau wa Elimu, Afya na Taasisi ya kutengeneza vitambulisho Nida ,Rita kwa lengo la kuangalia ni namna gani tunaweza kabiliana na changamoto ya kutunza data “Alisema Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Datalab Omary Bakari
Omary Bakari aliwataka wadau katika mafunzo hayo kuitumia vizuri fursa hiyo ili kuweza kuona maeneo ambayo yanahitaji kutiliwa mkazo ikiwamo na Serikali kuweza kuwekeza ili kuboresha matumizi ya data kwa maendeleo ya wananchi wake.
Mkurugenzi hiyo aliongeza kwa kusema kuwa endapo endapo data hazitatumika kwa uhakikakunaweza sababisha hasara kubwa na ili zisitokee ndio maana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji ameona ni vyema kuimarisha ukusanyaji wa data .
Kwa upande wake Mtakwimu wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Juma Mkombozi wanaimani na mafunzo hayo kuwa yatawawezesha watumishi pamoja na wadau mbalimbali kuweza kutambua umuhimu wa matumizi ya data kwaajili ya mipango na kufanya maamuzi mbalimbali .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.