Baadhi ya watendaji kata jijini tanga wamesema wametekeleza agizo la Mstahiki Meya wa Jiji Mustapha Seleboss la kutoa elimu juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona katika kata zao hususani kwa watoto ambao bado wanafanya mikusanyiko wakati wa kucheza bila kuchukua tahadhari .
wakizungumza na tanga television watendaji hao wamesema kuwa wametoa elimu katika kila kaya lakini bado uelewa umekuwa mdogo kwa wazazi kutokuchukua tahadhari kwa watoto wao.
“Sisi kama viongozi wa kata tumechukua hatua mbalimbali ambazo tuliambiwa na tumeongea na wenyeviti wa mtaa na kuwashauri wawaelimishe wazazi jinsi ya kuwalinda watoto wao juu ya janga hili “Alisema Afisa mtendaji kata ya majengo Peter Ruta
Sambamba na hayo afisa mtendaji huo alisema wametoa maagizo kwa watendaji wa mitaa kukutana na wananchi wao bila kutengeneza mikusanyiko mikubwa ili kuhakikisha suala la kuwazuia watoto wao kucheza katika mikusanyiko .
Nae afisa mtendaji kata ya Chumbageni Rehema Said amesema wamejaribu kuwahamasisha viongozi wa mitaa kuendelea kushirikiana katika kutoa elimu ili kuweza kuokoa nchi yetu katika janga la corona .
Mpaka kufikia sasa jumla ya wagonjwa waliogundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona kwa nchi yetu ni 20 ambapo serikali bado inaendelea kuchukua tahadhari zaidi juu ya kuendelea kujikinga na virusi hivyo .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.