Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka wananchiwa Jiji la Tanga hasa wakazi wa kata ya Pongwe kutekeleza Mikataba waliyoyopeana na Halmashauri ya Jiji hilo ya kujenga Vibanda katika stendi ya Pongwe .
Mwilapwa ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jiji la Tanga ambapo amewata wananchi hao kufanya vile walivyoahidiana na Halmashauri hiyo.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwilapwa amesema anaamini endapo watu wataitikia wito huo kazi itakamilika kwa haraka na kuleta maendeleo ya Jiji pamoja na pato la Taifa.
"Kama Serikali naweza nikasema natoa muda wa mwezi mmoja watu watekeleze mkataba tuliyopeana kwa ambaye hajaanza kabisa kujenga autumie huu mwezi kufanya hivyo tunatarajia hapa mahali pote pawe pameziba kwasababu Halmashauri imeshatekeleza yale ya kwake ya msingi kwaiyo natarajia ndani ya huo mwezi mmoja nipate taarifa kwamba nini kimefanyika",.Alisema Mkuuwa wilaya ya Pongwe Thobias Mwilapwa
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Ramadhan Possi amesema watahakikisha wanafuata maelekezo waliyopewa na Mkuu wa Wilaya kwa wale ambao watakuwa hawajatekeleza mikataba hiyo kunyang'anywana kupewa wengine.
Kwa upande wao wananchi wa kata hiyo wamesema wanapongeza hatua hiyo kwani wanaamini itawasaidia kwa asilimia kubwa katika kuleta maendeleo ya kata yao.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.