Kamishina jenerali wa jeshi la zimamoto na uokoaji nchini John Masunga amesema mikakati waliyonayo kwa sasa ni kuhakikisha Jeshi hilo linatoa huduma zenye ufanisi kwa Wananchi kote Nchini.
Kamishina Masunga ameyasema hayo katika ziara yake Mkoani Tanga ambapo ikiwa ni mwendelezo wa kuzunguka katika Mikoa mbalimbali na kuweza kuzungumza na Maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kusikiliza changamoto zao.
"Lengo la ziara yangu katika Mkoa wa Tanga kama mnavyojua niliapishwa na Mheshimiwa Rais tarehe 3 ya mwezi wa pili kuwa Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Nchini nazunguka katika Mikoa ili niweze kujua changamoto zinazowakabili Maofisa katika sehemu zao za kazi".,Alisema Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini John Masunga
Mbali na kusikiliza changamoto hizo pia Kamishina Masunga amewapa pole wananchi wa Mkoa wa Tanga Kwa kukubwa na mafuriko ambayo yameweza kuchukua baadhi ya watu na mali zao.
Sambamba na hayo pia Kamishina Jenerali Masunga ameeleza vitu ambavyo vinaweza kusababisha wao kama Jeshi la zimamoto na uokoaji kuweza kuchelewa kufika katika eneo la tukio kwa haraka.
"Kuchelewa kufika kwenye tukio kunasababishwa na vitu vingi kama taarifa kuchelewa kufika kwa haraka lakini pia umbali katika eneo lililotokea tukio hizi ndio sababu mojawapo ambazo tunaweza chelewa kwahiyo wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kwa haraka".,Alisema John Masunga
Kwa upande wake Erenest Kimaro ambaye ni Mkazi wa Jiji la Tanga amelipongeza Jeshi hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuokoa wananchi katika majanga mbalimbali.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.