Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli itahakikisha mali zote za Wakulima wa zao la Mkonge kote Nchini zinarudishwa mikononi mwao na hakuna mtu yeyote atakayeonewa .
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo wakati akifungua jengo la bodi ya mkonge lililopo Jijini Tanga ambapo amesema watafanya hivyo kwasababu Mkonge ni fedha hivyo Halmashauri zinatakiwa kuweka vitalu vya kuzalishia mbegu na kuwapa Wananchi bila kuwatoza fedha yeyote .
“Tutarudisha mali zote za wakulima na ninawahakikishia hakuna mtu yeyote atakayeonewa kama tulivyofanikisha kurudisha hizi mali za bodi ya Mkonge tutafanya hivyo kote bila kumuonea mtu yeyote na kuanzia leo bodi hii ya Mkonge imethibitishwa kuwa bodi kamili ,mkonge ni fedha hivyo Halmashauri wekeni vitalu mzalishe mbegu muwape wananchi bure kama una shamba kubwa hujaliendeleza kulingana na muda uliowekwa tutalichukua”Alisema Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Tanzania
Aliongeza kuwa Serikali imedhamiria kulirudisha zao hilo hivyo alitoa wito kwa Wananchi hususai wa Mkoa wa Tanga wajipange katika kuyafufua mashamba yao na kuanzisha mapya na Serikali itawasaidia kuhakikisha mbegu bora na pembejeo zinapatikana kwani amewahusisha wadau kutoka Taasisi mbalimbali za kifedha na kwamba Serikali imeweka utaratibu utakaowawezesha wakulima hao kupata mikopo .
“Zao la mkonge ni muhimu nchini kwani linawanufaisha wakulima wadogo ,wakati na wakubwa Mkonge wa Tanga ni uchumi kwa wananchi na ni mkombozi kwasababu unawawezesha kupata riziki zao kwani hapo katikati halikuwa na tija lilikuwa linalimwa na Mikoa zaidi ya 12 lakini sasa limeachwa kwenye Mikoa minne tu “Aliongeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Naye Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba Pamoja na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu walitumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mkuu kwa jitihada kubwa anazozifanya katika kusimamia sekta ya kilimo likiwemo zao la mkonge .
“Tukushukuru Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa kwa Uadilifu wako na uzalendo wako uliokufanya uunde kamati ya kuchunguza mali za bodi ya mkonge Tanzania na hatimae leo hii mali zao zimerudi “Walipongeza Mawaziri hao Omary Mgumba pamoja na Ummy Mwalimu
Nao Wakuu wa Mikoa ya Pwani Morogoro na Kilimanjaro waliishukuru Serikali kwa kulifufua zao hilo na kwamba wameshaweka mipango ya kuendeleza zao hilo na wameiomba Wizara ya kilimo ishirikiane nao kwa kuwasaidia wakulima katika kuendeleza zao hilo ikiwemo aandaaji wa mashamba ,uendelezaji pamoja na ufuatiliaji wa Masoko .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.