Katika Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani lililoongozwa na Mstahiki Meya Mhe. Abdurahman Shiloow Diwani wa Kata ya Mzingani aliyethibitishwa leo Disemba 15, 2020 kuwa Mstahiki Meya wa jiji la Tanga kwa kura zote za Ndiyo, amewakumbusha Madiwani kuwa wanadeni kubwa kwa wananchi wa Jiji la Tanga za kutimiza yale waliyoahidi ya kuwaletea Maendeleo na utatuzi wa kero zilizoko kwenye maeneo yao.
“tunajukumu la kuwasaidia wananchi kuwaletea maendeleo lakini na kuwatafutia ufumbuzi wa kero zao ,niwatake mwende mkawe sehemu ya majibu ya kero zao badala ya kuwa watazamaji tu bila kuchukua hatua stahiki za kumaliza kero hizo,” Alisema Mstahiki Meya.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanga ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo kabla ya kumchagua Mstahiki Meya Bi. Faidha Salimu aliwataka madiwani kwenda na kasi ya Maendeleo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Joseph Magufuli kwa kuhakikisha kila diwani katika Kata yake analeta Maendeleo kwa vitendo.
Aliongeza pia kuwa Madiwani wanawajibu wa kuwa walinzi wa amani kwenye maeneo yao kutokana na kuibuka kwa viashiria vya uvunjifu wa amani ikiwemo vitendo vya ukabaji na wizi.“waheshimiwa Madiwani nawaomba mkawe mabalozi wa kuhamasisha ulinzi na usalama kwani tayari tunataarifa za uwepo wa vikundi vya watu ambavyo vimeanza kutishia hali ya usalama kwenye maeneo yenu, hivyo kupitia nyie mtaweza kubadilisha hiyo hali,” Alisisitiza Katibu Tawala.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Tanga linaundwa na jumla ya madiwani 36, wa kuchaguliwa 27 na Viti maalum 9 kutoka kata ambao wote wametokana na chama cha Mapinduzi (CCM),watahudumu kwa kipindi cha miaka mitano (2020-2025).
Kushoto Mbunge wa Mkoa wa Tanga Mhe. Eng Mwanaisha Ulege, katikati Mbunge wa jimbo la Tangamjini Mhe.Ummy Mwalimu na kulia ni Diwani wa kata ya Mzingani ambaye ni Mstahiki Meya.
Wahe.Madiwani wakisikiliza kwa makini uwasilishaji wa Taarifa za utekelezaji kwa miezi 6.
Wahe.Madiwani wakisikiliza kwa makini matukio yanayoendelea katika Ukumbi.
Wahe.Madiwani wakila kiapo katika Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani.
Wahe.Madiwani wakisikiliza kwa makini uwasilishaji wa Taarifa za utekelezaji kwa miezi 6.
Wakuu wa idara wakiwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.