Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe.Ummy Mwalimu ameahidi kutoa ushirikiano kwa madiwani wote 27 wa kuchaguliwa na 9 wa Viti Maalum wa jiji la Tanga walioapishwa leo Disemba 15, 2020. Akizungumza na Madiwani hao Mhe.Ummy amesema kuwa wao kama viongozi wana kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi wa Tanga Mjini kwa kuwa wanaimani kubwa juu yao ya kuleta mabadiliko kwa kufanya kazi kwa juhudi kubwa. Aidha Mhe.Ummy amewaomba Madiwani kuhamasisha wananchi katika ujenzi wa madarasa ya ziada 44 ili watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021 waweze kuendelea na masomo yao.
Katika Mkutano huo Mhe.Ummy pia amewasisitiza Madiwani kuhakikisha wanalipa kipaumbele suala la utunzaji wa mazingira katika kata zao huku akiahidi kupambana na wale wote wanaotiririsha maji taka yenye sumu kutoka viwandani, na hawatasita kuwachukulia hatua wanaochukua miundombinu ya Serikali kwa kuifanya vyuma chakavu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makama wa Rais Mhe.Ummy Mwalimu ambaye ni Mbunge wa jimbo la Tangamjini.
Wahe.Madiwani wakiwa kwenye Mkutano wa Baraza wakisiliza yanayoendelea katika mkutano huo.
Wahe.Madiwani wakiwa kwenye Mkutano wa Baraza.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushiriki katika Mkutano wa Baraza.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.