Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (Council Management Team - CMT) ya Jiji la Tanga, leo Jumanne Juni 13, 2023, imefanya ziara ya kutembelea miradi mikubwa miwili inayotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni kwa lengo la kukagua hatua za utekelezaji na mipango ya usimamizi na uendeshaji wake.
Timu hiyo inayoundwa na Mkurugenzi wa Jiji pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Halmashauri, ilianza kwa kutembelea jengo la Kitega Uchumi Kituo cha Mabasi Kange, mradi ulio katika hatua za umaliziaji unaotegemewa kugharimu kiasi cha zaidi ya shillingi Billion 8.7 hadi kukamilika kwake(fedha za Serikali Kuu), na utaiwezesha Halmashauri kutoa huduma za kijamii na kiuchumi kwa wakazi wake.
Mradi wa pili ni ujenzi wa eneo la wazi la bustani ya Jamhuri Park, maarufu kama "Forodhan" ambapo mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu wa Juni, 2023, na ukitegemewa kugharimu kiasi cha shillingi Billion 1.8, fedha za wafadhili, Fondation Botnar.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.