Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ameipongezaTARURA kwa kutatua kero mbalimbali za barabara katikaJiji la Tanga .
Mwilapwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayosimamiwa na wakara wa Barabara mijini na vijijini TARURA Jijini hapa.
"Kwa ujumla barabara zetu zinazozunguka Jiji la Tanga kwa sasa zinahudumiwa na hii mamlaka Inaitwa TARURA tangu ilipopewa mamlakaya kufanya kazi hatufanyi kwaajili ya siasa tunafanya kwaajili ya watu ",.Alisema Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Kwa upande wake meneja wa TARURA Jiji la Tanga Bonifas Mwambene amesema kwa mwaka wa fedha 2019/2020 walikuwa na bajeti ya shilingi billion 3.07 ambazo wanatarajia kutengeneza barabara za vumbi na lami .
Sambamba na hayo pia Mwambene amesema uboreshaji wanaoufanya ni uboreshaji wa kawaida ambao utasaidia kupitisha mabasi makubwa na madogo.
pia mwambene amewata wananchi wa Jiji la Tanga kuwa watunzaji wa miundombinu yabarabara ya Jiji hilo.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.