Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini kwa kushirikiana na wizara ya Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imezindua kituo cha muda cha kutoa huduma ya methodone kwa waraibu wa dawa za kulevya aina ya heroine.
Akizindua kituo hicho katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu aliweza kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali katika mapambano dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
Waziri Ummy aliongeza kwa kusema kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa tiba kwa waraibu wa dawa za kulevya imezindua kituo hicho cha muda ikiwa ni katika kutekeleza mpango wake wa muda mfupi ili kuweza kufikisha huduma kwa walengwa.
“Ukiangalia changamoto kubwa katika Mkoa wa Tanga ni dawa za kulevya mimi nitoe wito kwa Wananchi kuwa Mkoa wetu ni mzuri kwasababu unafursa zote za kimaendeleo kiuchumi kwaiyo endapo tutashirikiana tutaondoa Tanga katika nafasi ya pili kwa matumizi ya dawa za kulevya”Alisema Ummy Mwalimu
Ummy amesema kupitia mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya inawataka Wananchi kushirikiana na asasi na wadau wengine katika kuwashawishi waathirika wa dawa za kulevya waweze kufika kwenye kituo hicho kupata huduma na tiba pamoja na ushauri.
Uzinduzi wa kituo hicho ni muendelezo wa vituo vungine vilivyopo Nchini kwani mpaka sasa kuna vituo 8 ambavyo vinatoa huduma kila siku kwa Waraibu 8500 ambapo vitatu vipo Dar es salaam ,Mbeya ,Mwanza ,Pwani na Jjijini Dodoma .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.