Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa corona kama Serikali inavyosisitiza kufuata taratibu zinazoelezwa na wataalamu wa Afya .
Seleboss amesema kuwa Mkoa wa Tanga unamwingiliano na Mkoa wa Arusha Katika suala la usafiri na tayari wameshaandaa maeneo ya kupokea wagonjwa wa Corona pindi watakapotokea lakini pia timu ya madaktari wameshaandaliwa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa watakaopatikana .
"Wanatanga hatupo mbali sana na Arusha lazima tuchukue tahadhari mapema Usafiri unaotaka Tanga unafika siku ileile Arusha na yanayotoka Arusha yanafika Tanga siku hiyohiyo kwaiyo niwaombe wanataka tuwe na mshikamano wa pamoja na kumwomba mwenyezi Mungu atuepushe na janga hili"Alisema Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss
Seleboss ameongeza kuwa wao kama Serikali wameshaanza kuchukua tahadhari mapema Kwa kuandaa maeneo ya kuwapoke wagonjwa watakaodhibitika na ugonjwa huo pia wameandaa timu pamoja na vifaa tiba .
Pia Seleboss amesema wao kama Halmashauri wamemeanza mchakato wa kusafisha makomeo ya milango katika ofisi zao pamoja na kuandaa vifaa vya kusafishia mikoni ili kujiweka katika tahadhari ya corona.
Mbali na hayo amewataka wananchi kuwa na utii wa maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya pamoja na kuwapa pole kwa familia ambazo zimeshapata wagonjwa hao.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.