Wakuu wa idara mbalimbali kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wamefanya ziara ya kujifuza na kuona namna ambavyo Jiji la Tanga linavyoendesha shughuli za ukusanyaji wa mapato na kuipongeza Halmashauri hiyo kwa jinsi ilivyoweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi .
Akizungumza na Tanga televisheni mchumi wa kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam John Marcello alisema kuwa wamefurahishwa na miradi waliyoiona hasa mradi wa kiwanda cha matofari.
“Tumekuja kujifunza uendeshaji wa stendi katika Jiji la Tanga hususani katika mfumo ambao unatumika katika ukusanyaji wa mapato yanayopatikana katika stendi tunataka tujifunze ili tutakapoanze tuanze vizuri “Alisema John Marcello
Sambamba na hayo pia aliwapongeza wasimamizi wanaosimamia katika ukusanyaji wa mapato kwa kuwa waaminifu katika kazi yao .
Mbali na hayo pia John Marcello aliwezakuahidi kuwa wataendea kuyafanyia kazi ili kuweza kuinua uchumi wan chi pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali .
Lengo la Wakuu wa idara mbalimbali kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kufanya ziara katika Jiji la Tanga ni kuona namna ambavyo Halmashauri hiyo itekeleza majukumu yake ambapo imeweza kutembelea Jengo jipya la Halmashauri hiyo ,kituo cha mabasi cha kange,kiwanda cha matofali pamoja na dampo .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.