Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kupata hati safi kwa awamu nne mfululizo.
Shigela aliwasisitiza watumishi wa Halmashauri kuwa na weledi mkubwa kipindi ambacho Baraza la Madiwani litakapo maliza muda wake ili watakaporejea tena wakute mambo yanakwenda vyema.
Shigela aliongeza kwa kuwatoa hofu Madiwani kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipanga katika kuhakikisha Madiwani hao wanapata kiinua mgongo .
“Ninauhakika awamu itakayokuja mtajipanga vizuri kutafuta viongozi waliobora watakaoendeleza gurudumu hili na mimi nafarijika kuwa mnakwena kwenye uchaguzi hamuidai Halmashauri hakuna posho inayodaiwa “ Alisema Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela
Kwaupande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss aliwapongeza Madiwani hao kwa kazi nzuri ambazo wamekuwa wakizifanya bila kuangalia itikadi zao za vyama na kuamua kuwatumikia wananchi wao.
“Kuheshimiana kwetu na utulivu ushirikiano ambao tumekuwa nao ndio umesababisha kusaidia kupata hati safi ambayo tumeipata”Mustapha Seleboss alifafanua
Halmashauri ya Jiji la Tanga imefanikiwa kuchukua hati safi katika ukusanyaji wa mapato kuanzia mwaka 2017 mpaka 2020 mfulilizo
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.