Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Tanga imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilling milioni tatu laki sita na sitini na nane elfu ambazo zilikuwa zimetumika kinyume na sheria na kanuni sahihi za matumizi ya fedha za umma pamoja na kudhibiti kiasi cha shilling milioni kumi na tano laki tatu na tisini elfu.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga Dkt Sharifa Bungala wakati akitoa taarifa kwa kipindi cha mwezi januari mpaka machi 2020 .
Dkt Sharifa aliongeza kuwa katika kipindi hicho pia walifanikiwa kudhibiti kiasi cha shilingi milioni moja laki saba na tisini na nne elfu zilizotokana na kukamatwa mbao ambazo zilivunwa bila kibali na Serikali ya kijiji cha Mseko katika Wilaya ya Pangani .
“Mtu aliomba kibali cha kuvuna mbao chache lakini akaenda akavuna mbao nyingi tofauti na zile ambazo alitakiwa avune ambazo alikuwa hajazilipia kodi na vibali mbalimbali pamoja na tozo kwaiyo tumedhibiti na hizo pesa zimepatikana “Alisema Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga Dkt Sharifa Bungala
Sambamba na hayo pia taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Mkoa wa Tanga tumefanikiwa kuelimisha na kuhamasisha umma kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi machi 2020 kwa wanafunzi wa elimu ya msingi ,sekondari pamoja na vyuo vikuu na kufanikiwa kuimarisha klabu 148 na kufungua klabu mpya 13
Pia Dkt Sharifa aliongeza kwa kusema mipango mikakati yao katika kipindi cha mwezi april hadi juni mwaka 2020 wanategemea kuendelea kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi kuongeza ushiriki ao katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.