Taasisi ya African Muslim Agency Jijini tanga yawezesha upatikanaji wa visima vya maji katika maeneo muhimu jijini Tanga.Mradi huo wa visima vya maji umezinduliwa siku ya jumatatu 16.04.2018 katika bustani ya “Korogwe road” na soko la Ngamiani, visima hivyo vitachangia sana usafi wa jamii kwa ujumla na ukuaji wa uchumi na mabadiliko yake, lakini pia vitachangia kubadilisha na kuleta maisha bora kwa jamii ya wengi na hasa wadau wa maeneo hayo.
Aidha Mkurugenzi wa Jiji la Tanga alisema visima hivyo vitatunzwa, vitatumiwa, vitaendelezwa, vitaboreshwa, vitasimamiwa na kudhibitiwa kwa kuzingatia kanuni muhimu za matumizi ya maji kwa kuzingatia sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji na. 11 ya mwaka 2009.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Jiji la Tanga alitoa shukran za dhati kwa Mkurugenzi wa taasisi ya “African Muslim Agency” na pia ombi la kuendeleza ushirikiano uliopo ili kufanikisha azma ya kuwezesha upatikanaji wa maji ya uhakika katika maeneo yote yenye uhitaji huo.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.