Mkuu wa wilaya ya Tanga Mheshimiwa Hashim Mgandilwa amewaongoza wakazi wa Jiji la Tanga katika maadhimisho ya siku ya usafi wa mazingira duniani yaliyofanyika Septemba 17, 2022 ambapo kwa Jiji la Tanga maadhimisho hayo yamefanyika kwa kufanya usafi katika fukwe za bahari maeneo ya Deep Sea na Kasera Fish Market.
Akiongea baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Mgandilwa amewataka wananchi kutotupa taka kwenye fukwe ili kulinda usalama wa viumbe hai pamoja na kuimarisha uchumi unaotokana na bahari. Amesema kuwa wakazi wa Jiji la Tanga wanategemea kitega uchumi cha bahari katika kufanya shughuli zao hivyo ni vyema kufanya usafi katika maeneo hayo ili kunusuru viumbe wa bahari.
Kwa upande wake Afisa mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Tanga ndugu Kizito Nkwabi amesema maeneo yote ni muhimu katika kuyafanyia usafi hivyo kila mwananchi anao wajibu wa kushiriki katika zoezi hili. Kizito amesema kila mwananchi anazalisha taka hivyo ni lazima awe na chombo cha kuhifadhia taka na kuepuka kutupa hovyo taka hizo ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.
Nao baadhi ya wadau waliohudhuria katika usafi wa fukwe za bahari wamesema ni vema kulinda mazingira ya fukwe kwani taka zinaweza kuleta sumu kwa viumbe wa bahari hata kuleta madhara kwa binadamu.
Aidha wametoa wito kwa wananchi wote wa jiji la Tanga kutunza mazingira na kudumisha usafi ili kuweza kukuza kipato cha taifa
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.