Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Bw. Mustapha Seleboss ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uongozi ya Jiji, amewataka mafundi wanaojenga na wataalam wanaosimamaia ujenzi kwenye vituo vya afya kuongeza kasi ili kumaliza miradi hiyo ndani ya wakati. Mstahiki Meya, aliyasema hayo leo akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na kamati hiyo jijini humo.
Mstahiki Meya aliongeza kwa kusema ya kwamba, kama ikiwezekana mafundi kufanya kazi hadi usiku, halmashauri tupo tayari kuwawekea taa ili kazi iendelee na kukamilika kutokana na maelekezo ya serikali kuu. “Nawaomba sana tuongeze kasi kwenye kujenga miradi hii ili tumalize kwa wakati kama ilivyoelekezwa na serikali kuu” alisema.
Pamoja na msisitizo wa kumaliza kazi ndani ya muda, kamati hiyo imewakumbusha wataalam kujipanga kuongeza miundo mbinu ya umeme, maji safi na maji taka kwani matumizi ya huduma hizo yataongezeka baada ya kukamilika na kuanza kutumika kwa majengo hayo. Aidha, kamati hiyo iliwataka wajumbe wa Kamati za Manunuzi na Mapokezi kwa kila mradi ambazo ndizo zinazosimamia shughuli za ujenzi, kuendelea kuwa karibu na miradi hiyo kwa kuhakikisha wan taarifa ya kila kinachongia, kiwango cha pesa kilichotumika na na hatua aliyofikiwa kwenye eneo la mradi.
Serikali kuu imetoa jumla ya Tsh. Bilioni 1.4 kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kufanya upanuzi wa vituo vya afya vitatu vya Mikanjuni, Ngamiani na Makorola, upanuzi huo unalenga kujenga majengo yatakayo tumika kama wodi ya watoto, wodi ya wanawake wazazi, vyumba vya upasuaji na vyumba vya kuhifadhia maiti kwenye kila kituo cha afya.
Kamati ya Fedha na Uongozi ni moja ya kamati za kudumu kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga, pamoja na majukumu yake mengi, moja ya majukumu yake ni kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na halmashauri. Kamati hii inaongozwa na Mstahiki Meya ikiwa na wajumbe tisa. Kwenye ziara hii kamati hiyo ilitembelea na kukagua jumla ya miradi nane, ikiwemo Kituo cha Afya Mikanjuni, Kituo cha Afya Makorora, Kituo cha Afya Ngamiani, Shule ya Msingi Bombo, Shule ya Sekondari ya Mkwakwani na Shule ya Msingi Kiomoni
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.