Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe Abdulrahman Shiloow amewataka watendaji wa kata kwa kushirikiana na watendaji wa mitaa, kuhakikisha wanaondoa mifugo inayozagaa na kuzurura ovyo katika maeneo yao na kuihamishia pembezoni mwa mji ili kuhakikisha sheria ya majiji inazingatiwa.
Mhe shiloow amesema hayo katika mkutano wa baraza la madiwani la kupokea taarifa za kata uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
“Kata ya Makorora, Mzingani mifugo inazurura tu, Watendaji mtusaidie mkashirikiana na watendaji wa mitaa kuhakikisha mifugo inayorandaranda mitaani na kuharibu bustani za watu mnaikamata na kuipiga faini” amesema Mstahiki Shiloow
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana ameongeza kwa kusema kuwa Jiji halihitaji mifugo inayochungwa.
“Tunahitaji mifugo inayofugwa ndani, hatuhitaji kuchafuliwa mazingira. Watendaji simamieni maeneo yenu, kamateni mifugo mkishindwa tutawapiga nyie faini “ amesisitiza Dkt. Liana.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.