Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini leo amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa unaondelea katika Shule 10 za Sekondari zenye upungufu wa Vyumba vya Madarasa 31 na kuongeza ziada 13, na Kufanya jumla ya Madarasa yanayojengwa 44 kati ya Shule za Sekondari 26 za jiji la Tanga ambazo ni Toledo Sekondari,Pongwe Sekondari, Japan Sekondari, Kihere Sekondari, Horten Sekondari, Mikanjuni, Mnyanjani, Chumbageni na Macechu Sekondari ikiwa ni Shule iliyounganisha kata 3( Majengo,Central na Chumbageni).
Mhe.Ummy Mwalimu akiwa katika ukaguzi huo ameshiriki katika kuchimba Msingi wa vyumba vya Madarasa Shule ya Sekondari Mwapachu ikiwa ni kuunga mkono juhudi za ujenzi huo ili kuhakikisha Wanafunzi 6,662 waliofaulu kujiunga kidato cha Kwanza Januari 2020 wanapata nafasi ya kusoma.
Aidha Mhe.Ummy Mwalimu ameahidi kutoa Tsh.Mil 8.4 kutoka kwenye Mshahara wake ili kununua mifuko ya 600 ya Simenti huku akisisitiza kutumia mfuko wa Jimbo kununua Madawati kwa Shule hizo.
Akiwa katika ukaguzi huo Mhe.Ummy Mwalimu Mbunge wa Jimbo la Tanga ameipongeza Halmashauri ya jiji la Tanga kwa kutoa Tsh.Mil 288 za Mapato ya ndani na kuelekeza kwa kasi kwenye ujenzi wa vyumba vya Madarasa, pia amewapongeza Wananchi kwa kujitoa na kuunga juhudi za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.