Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amekishukuru chama cha usafirishaji abiria Mkoa wa Tanga (TAREMIA) kwa kutoa msaada wa vifaa vya kunawia mikono Madumu (22) kama jitihada za kuunga mkono Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona katika stendi nne zilizopo Jijini Tanga.
Akiwashukuru Wasafirishaji hao Mwilapwa amesema kuwa mpaka hivi sasa Tanga haijapata mshukiwa yoyote wa virusi vya corona kwani wahudumu wa afya wanatoa elimu kwa jamii kwa kuzingatia usafi pamoja tahadhari zote zinazotolewa na serikali.
“Na mimi nakili kupokea na ninawashukuru sana kwamba somo lilieleweka zaidi ya kutoa elimu mumekusanyanya na kuchanga mlichobalikiwa ili muweze kutoa msaada katika vituo kama mlivyosema kila katika kituo cha usafiri mmeweza kutoa na chombo cha maji ya kutililika “,.Alisema Thobias Mwilapwa
Mbali na shukrani hizo pia Mkuu wa Wilaya huyo aliwataka wananchi kuzingatia maagizo wanayopewa hasa wasafiri na vyombo mbalimbali .
Sambamba na hayo pia amewataka makonda kupunguza tabia ya kuwajaza abiria katika daladala na kuwataka kufuata agizo la kukaa usawa wa siti zilizopo ili kuweza kuendelea kujikinga na ugonjwa wa corona .
Kwa upande wake mwenyekiti na katibu wa chama cha usafirishaji abiria mkoa wa tanga Ismaili Masudi na Juma Kipingu wamesema lengo la kutoa msaada ni kuhakikisha wananchi wa Jiji la Tanga hawapati maambukizi ya virusi vya corona .
“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya hili zoezi lote ni maagizo yako kwaajiliya kuwasaidia Wananchi wa Jiji la Tanga pamoja na abiria wetu ambao wanasafiri kwenye stendi zetu nne kwani hivi vyombo vinakwenda katika stendi hizo “,.Wamesema viongozi wa chama cha usafirishaji abiria Mkoa wa Tanga
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisema kuwa kutokana najitihada zinazofanywa na wadau pamoja na Serikali juu ya kupiga vita ugonjwa wa corona Jiji la Tanga Litashinda .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.