Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe .Martine Shigela amewataka wananchi wa kata ya Tangasisi ambao wana migogoro ya ardhi kujitokeza na kutoa vielelezo ili wapewe haki zao.
Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika kata hiyo na kata zote 27 za jiji Tanga.
Mhe. Shigela amesema kuwa kila mwananchi ambae anavielelezo vya umiliki wa eneo anatakiwa kuvitoa ili kupewa haki anayostahiri na kama hana haki ya kupewa aandikiwe barua inayoeleza kuwa hana haki ya eneo hilo kwa mujibu wa sheria.
“nitatuma watu wangu kutoka mkoani na vyombo vya dora waje waweke kambi ya wiki nzima hapa wamusikilize mtu mmojammoja atoe vielelezo vyake na kama anahaki wamuandikie haki yake anayostahiri kupewa na kama eneo lake haki yake haipo aandikiwe barua ya majibu kwamba kwa mujibu wa kifungu hiki tumejilidhisha haki yako haipo kwa sababu eneo hilo ni mali ya mtu mwingine “amesema Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe .Martine Shigela.
Pia amemtaka Diwani wa kata hiyo kupita na kutangaza kwa wananchi kuwa wale wote wenye migogoro ya Ardhi walioiwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa kuwa wataalamu watakuwepo katika Ofisi ya kata kuanzia tarehe watakayo tangaza na kuwapanga waende kimitaa ili kurahisisha kazi hiyo.
“Nikuombe Mhe Diwani wa Kata hii wataalamu Wa Kupamba Ratiba ya kupita kata kwa kata, gari la matangazo limite na kuwatangazia wananchi kuwa kuanzia tarehe fulani wataalamu watakuwepo kwaiyo wote mliotoa malalamiko yenu kwa Mkuu wa Mkoa jitokezeni na vilelezo vyenu na kuwapanga wajitokeze kwa Kila Mtaa “ameyasema hayo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe . Martine Shigela .
Akihitimisha ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martine Shigela amewataka Maafisa Ardhi kuweka kambi kila kata ili kutatua migogoro ya Ardhi ambayo imeonekana kukithiri katika Jiji la Tanga na baada ya kukamilika ripoti ya utatuzi wa migogoro hiyo ifike Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.