Vijana wa Jiji la Tanga wametakiwa kucheza michezo ya asili na kuacha kupoteza muda mitandaoni ili kudumisha utamaduni wa asili zao.
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe.Mustafa Selebosi wakati wa uzinduzi wa michezo ya asili iliyofanyika katika kata ya Nguvumali iliyopo jijini Tanga,lengo la michezo hiyo ni kuwajengea uwezo vijana kuzitambua tamaduni zao.
Akizindua michezo hiyo waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amesema kuwa bonanza hilo linazungumzia mambo makubwa matatu ikiwemo michezo ni furaha, amani pamoja na ushirikiano hivyo amewapongeza kutokana na bonanza hilo kwani litatoa fursa ya kufurahi na kushirikiana pamoja.
Amempongeza muandaaji wa Bonanza hilo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi kwa kushirikisha vikundi kutoka kata mbalimbali za Jiji hilo na sio nguvu mali peke yake nakusema kuwa Tanga linapokuja suala la Maendeleo ya Tanga wanakuwa mstari wa mbele .
Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni pamoja na ngoma za utamaduni ,kama rede ,nyakwa, kachurana kioo na Mhe Ummy Mwalimu aliweza kupendekeza mchezo mmoja wa kombolela uchezwe katika bonanza hilo kwa atakaeshinda katika michezo hiyo mshindi wa kwanza atapata fedha taslimu kiasi cha shilingi laki mbili, mshindi wa pili laki na nusu ,na mshindi wa Tatu laki moja.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.