Mkuu wa Wilaya Tanga, Mhe. Thobias Mwilapwa hivi karibuni aliwaongoza watumishi wa serikali, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na wananchi katika zoezi la upandaji miji. Zoezi hilo ambalo lilifanyika kwenye eneo la shamba la miti na hifadhi ya mazingira Mleni lililopo pembezoni kidogo mwa Jiji la Tanga liliungwa mkono na Mkurugenzi wa Jiji hilo pamoja na wakuu wake wa idara.
Jumla ya miche ya tiki 2500 ilipandwa katika eneo la ekari tatu (3) kati ya ekari nane (8) lililotayarishwa. Upandaji utaendelea kwa kipindi chote cha mwaka. Akieleza faida za mradi huo Afisa Maliasili wa Jiji la Tanga bw. Aneny Nyirenda, ambaye ni msimamizi mkuu wa shamba hilo aliseme “Mbali ya kutoa ajira kwa wananchi, mradi huu una faida nyingine nyingi kama; Kutunza mazingira kwa kuongeza hifadhi ya hewa ya kaboni (carbon stock), kutumika kama Shamba darasa linalohamasisha watu kupanda miti yenye thamani na ufugaji wa nyuki, Kulinda aridhi ya Umma dhidi ya wavamizi na pia ni Kitega uchumi cha Halmashauri ya Jiji yaani ni moja ya rasimali muhimu”.
Eneo la shamba lina ukubwa wa Ekari 161 lilitwaliwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira kutokana na hali ya jangwa inayolikabili eneo hili. Kwa kipindi chote shamba hili liliachwa vichaka vya asili. Mnamo mwaka 2009 Halmashauri iliamua kuliendeleza kwa kupanda miti ya Tiki, ambapo hadi sasa ekari 41.5 zimepandwa jumla ya miti 40,150.
Shughuli nyingine zinazofanyika katika shamba hili ni ufugaji wa nyuki na hadi sasa kuna mizinga 8 ya nyuki. Mizinga hii ina uwezo wa kuzalisha lita 320 za asali kwa mwaka.
|
|
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.