Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. OMARY MGUMBA amewataka maafisa na wajumbe wa kamati ya lishe Mkoa kuhakikisha wanawasaidia wananchi na Watoto chini ya miaka mitano kuwa na lishe bora na kuwaondoa katika hatari ya kupata udumavu katika Maisha yao.
Akizungumza wakati wa kikao cha utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe kwa kipindi cha mwaka 2021/2022, MGUMBA amesema kuwa taarifa zote za ulaji mzuri wa chakula zibandikwe katika mbao zote za taasisi za serikali kwa ngazi zote.
Aidha mgumba amesema kuwa halmashauri zote zitenge fedha zitakazo tumika kuboresha lishe kwa watoto wenyewe umri chini ya miaka mitano ili kuwakinga na maradhi.
Kwa upande wake, Mganga mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt. JONATHAN BUDENU amesema lengo ni kuwasilisha matokeo ya viashiria vya lishe ni moja ya utekelezaji wa agizo la serikali katika kuwahudumia wananchi wake.
Naye afisa lishe mkoa wa Tanga MWANAMVUA ZUBERI amesema asilimia 35 ya vifo vinatokana na lishe duni.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.