Flora Maingu, Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. HASHIM MGANDILWA amewaonya vikali wazazi na Walezi Jijini Tanga ambao bado hawajawapeleka Watoto wao shule walio chaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Jiji la Tanga kuwa Hatua kali zitachukuliwa , kwa kutotimiza Majukumu yao.
Mgandilwa ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kushitukiza ya nyumba kwa nyumba katika Kata ya Chongoleani kusaka Watoto ambao hawajaripoti shule,lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mtoto katika Wilaya hiyo anapata haki yake ya Msingi ya Kupata Elimu.
Hatua hiyo imefikiwa na Mkuu huyo wa Wilaya baada ya Kubaini kuwa Idadi ya Wanafunzi waliofika Shule kuwa ni ndogo ikilinganishwa na Idadi ya Waliochaguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari.
Viongozi mbalimbali wa kata hiyo akiwemo diwani Mhe. MWAVESO MBEGA wameahidi kuunga mkono jitihada za Mkuu huyo wa Wilaya ili kuhakikisha Watoto wote wanafika shule.
Jumla ya wanafunzi 31 ndio waliofika shule kati ya wanafunzi 1oo waliochaguliwa katika shule ya sekondari Ndaoya kata ya Chongoleani.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.