WASHIRIKI WA MAFUNZO YA MFUMO WA KUBORESHA TAKWIMU ZA CHANJO MKOA WA TANGA (TIMR) WAKIWA
KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO.
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto chini ya kitengo cha chanjo (IVD)
imekuwa ikishirikiana na shirika la PATH kutekeleza mpango wa uboreshaji wa Takwimu za
chanjo katika baadhi ya Mikoa hapa nchini.Katika uboreshaji huo wizara kwa kushirikiana
na shirika la PATH inaendesha mafunzo ya Mfumo wa Tanzania immunization Registry(TIMR).
Mafunzo hayo yanaendeshwa katika Halmashauri ya mji wa Korogwe kuanzia tar 10-14/07/2017 na
yanashirikisha wilaya zote za Mkoa wa Tanga.Mfumo huo wa TEHAMA utatumia Tablets katika kusajili
takwimu za utoaji chanjo katika vituo vya Afya na Zahanati.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.