Mussa Labani, Tanga.
Naibu Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Mwanaidi Kombo Chombo, leo, alhamisi Desemba 22, 2022, ameongoza kikao kazi cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Tanga lililopokea uwasilishaji wa elimu ya lishe juu ya umuhimu wa chakula mashuleni.
Mheshimiwa Chombo amesema suala la lishe ni la kitaifa, na mikataba ya usimamiaji wa shughuli za afua za lishe imesainiwa kuanzia ngazi ya Taifa hadi kwenye mitaa, katika ngazi ya Taifa ikishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akiwasilisha mada juu ya umuhimu wa chakula shuleni, Afisa Lishe wa Jiji la Tanga, Bi. Sakina Mustafa ametaja faida za lishe mashuleni kuwa ni pamoja na Wanafunzi kujifunza vizuri wakiwa wamekula ama kupatiwa chakula shuleni
Amesema chakula kinapoandaliwa Shuleni kinakuwa katika hali ya usalama kwa kuwa eneo lililoandaliwa Chakula linafahamika
"Wanafunzi wanaopata chakula shuleni wanakuwa rahisi kuelewa na kujifunza waliyo fundishwa na walimu wao. Uwepo wa chakula shuleni huongeza vichocheo vya kuamsha ari ya kuwahi na kuhudhuria shule na pia kupenda kusoma, na hupunguza utoro hasa shule za kata ambazo hazina uzio" Amesisitiza Bi. Sakina.
Kwa upande wao, baadhi ya madiwani wameahidi kwenda kuwaelewesha wazazi/walezi umuhimu wa chakula shuleni ili waweze kuchangia gharama za chakula.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.