Halmashauri ya jiji la Tanga imeendelea kupambana na maambukizi ya virusi vya homa kali ya corona ambapo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss amewataka madiwani kuwa mabalozi na kuendelea kuwaelimisha wananchi dhidi ya kujikinga na ugonjwa huo.
Seleboss ameyasema hayo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani ambapo kikao hicho kimefungwa kwa kuliombea taifa.
“Naamini serikali imetoa taarifa ya kuzuia mikusanyiko katika maeneo yote yenye mikusanyiko kwa lengo la kupambana na ugonjwa wa corona sisi kama Halmashauri tumeliona hili na tumelipokea na kuviandaa vyombo vyetu na ndio maana leo tunaendelea na kikao hiki tukiamini taratibu zote zimefuatwa kama kuweka mashine za kupima pale nje na kuhakikisha hakuna mtu anaingia bila kupima pale nje “,.Alisema Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss
Sambamba na hayo pia mstahiki meya huyo ametoa angalizo kwa wakazi wa pwani kuweza kujizuia na kujikinga katika upigaji chafya ili mate yasiweze kuwapata wangine na kumtanguliza mwenyezi Mungu kwa kila jambo wanalofanya .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka madiwani hao kusikiliza maelekezo wanayopewa na Serikali ili kuweza kushinda katika vita ya gonjwa la corona .
“Niwaombe waheshimiwa Madiwani kuwa wasikivu kwa Serikali katika mambo tunayoambiwa karibu maeneo mengi tunayoambiwa tuchukue tahadhari tufanye hivyo na tuwahamasishe wananchi kuwa wasafi “,.Alisema Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Mwilapwa ameongeza kwa kuwataka viongozi hao kushirikiana na serikali kwa kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kufahamu kuhusu ugonjwa wa corona .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.