Julai 11, 2024.
Halmashauri ya Jiji la Tanga kupitia Kitengo cha Fedha na Uhasibu, leo alhamisi, Julai 11, 2024, imeendesha mafunzo ya siku moja kwa kikosi kazi cha ukusanyaji mapato, yenye lengo la kuwajengea uelewa wa vyanzo vya mapato vinavyotarajiwa kukusanywa kwa mwaka huu wa fedha, 2024/2025, sheria zinazosimamia ukusanyaji wa vyanzo hivyo, matumizi ya mifumo ya ukusanyaji wa mapato, utoaji wa elimu na kauli za staha katika utekelezaji wa zoezi hilo.
Mafunzo hayo ambayo yalifunguliwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mhe. Abdulrahman Shiloow na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Jiji, Dkt. Frederick Sagamiko, yaliendeshwa na Mweka Hazina wa Jiji, Bw. Rumadha Mhando, ambapo Wakuu wa Idara na Vitengo wenye vyanzo vya mapato waliwasilisha mada juu ya vyanzo vya mapato vilivyo chini ya Idara/Vitengo vyao, sheria mama na sheria ndogo zinazotumika katika ukusanyaji, na washiriki kupata muda wa kujadili.
Kikosi kazi hiki, kinatarajiwa kuiwezesha Halmashauri kutimiza lengo lake la makusanyo, ambapo katika Mpango na Bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Halmashauri imepanga kukusanya kutoka vyanzo vyake vya mapato ya ndani kiasi cha shillingi Billion 21.3.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.