Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa amesema Halmashauri imechukua hatua ya kutatua changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2020.
Akizungumza na Tanga Television Afisa Elimu huyo amesema kuwa Halmashauri itajazia pale ambapo kuna mapungufu kwa kutoa matofali na mabati huku majukumu mengine yakielekezwa katika kata husika.
Gwakisa amesema kuwa vyumba vya madarasa vinahitajika kwaajili ya kukaa wanafunzi 4668 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza .
“Sisi Halmashauri katika shule hizi 10 tulisema tutatoa tofali kwakila shule kulingana na idadi ya madarasa ambayo yatahitajika sio tofali tu pia tutatoa bati pamoja na mbao kwaajili ya ujenzi wa madarasa hayo “,.Alisema Lusajo Gwakisa Afisa Elimu Sekondari Jijni Tanga
Sambamba na hayo Gwakisa amewataka wananchi kuongeza nguvu ili kukamilisha jambo hilo kwani ili kuhakikisha maendeleo ya wanafunzi yanakuwa mazuri lazima kuwe nausimamizi mzuri kutoka kwa wananchi wenyewe ikiwa ni pamoja na miundombinu wakiongozwa na Madiwani ,na wataalamu waliopo kwenye kata.
Halmashauri ya Jiji la Tanga imetekeleza agizo la Serikali la kutaka wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza Elimu ya Sekondari kuanza pamoja masomo hayo .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.