Halmashauri ya jiji la Tanga imesema itatoa boti kwa ajili ya kutatua kero ya kuvuka kutoka kijiji cha Mwalongo kuelekea Tongoni kutokana na eneo hilo kuzungukwa na ukanda wa bahari.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa jiji la Tanga Daudi Mayeji wakati akijibu kero ya wananchi katika ziara ya mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela anayofanya katika kata zote za jiji hili.
Daudi Mayeji amesema kama mashine imechoka watafuatilia wao kama halmashauri na watanunua mashine nyingine ili watoto waende shuleni bila shida.
“Eneo jingine ambalo ningependa kulizungumzia ni kuhusiana na kivuko kibovu kwa sababu linagusa maisha ya watu kama ishu ni mashine imechoka tutaifuatilia halmashauri itaangalia uwezekano wa kununua ili watoto wasipate shida wanapoenda shule “amesema Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
Ameongeza kuwa jambo hilo wamelichukulia katika mfumo wa dharura kwa sababu hawataki kifo chochote kiweze kutokea ndiyo waanze kuchukua hatua.
Pia ameongeza kuwa eneo la Tongoni kuna uvuvi haramu ambao unaendelea na madhara ya uvuvi huo yanaweza kusababisha vifo kwa baadhi ya watu kwa sababu sumu hiyo inafanya kazi polepole katika mwili wa binadamu.
“madhara yake wewe huwezi kuyaona saivi ,serikali inakuwa chungu katika suala la uvuvi haramu ukafikili kwamba inakinyongo na wananchi haina , kinachofanyika pale ni kwamba inajaribu kuokoa maisha ya wananchi ambao ni sisi wenyewe”Alisisitiza Mkurugenzi.
Uvuvi haramu ni jambo ambalo linatakiwa kukemewa na kuchukuliwa hatua za kisheria hivyo wavuvi wanapaswa kufuata sheria za uvuvi ili kuondokana na kesi zisizo za lazima.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.