UFAHAMU MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI KUTOKA HOIMA NCHINI UGANDA HADI BANDARI YA TANGA-TANZANIA
Mradi huu wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga Tanzania Unajulikana kama East African Crude oil Pipeline (EACOP).
Bomba hili litakuwa na urefu wa kilometa 1,445.
Mradi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kupitia Tanzania ulitangazwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakati wa Mkutano wa 13 wa ushoroba wa kaskazini ambapo alieleza kuwa Bomba hilo la Mafuta kutoka Hoima Ziwa Albert nchini Uganda litapita katika ardhi ya Tanzani kwenda bandari ya Tanga.
Aidha baadhi ya sababu zilizochangia bomba hilo kupita nchini ni pamoja na:
i. Ubora wa bandari ya Tanga ambayo imeonekana kuwa bora zaidi ukilinganisha na bandari nyingine Africa Mashariki kwa kuwa ina kingo za asili (naturally sheltered) na kina cha futi 25 kwenda chini hivyo kupunguza muda na gharama za ujenzi kwa kuwa uchimbaji wa kina hauhitajiki.Aidha bandari hiyo itakuwa na uwezo wa kupakia mafuta katika mwaka mzima.
ii. Miunganiko ya njia za reli ya Tanga hadi reli ya kati
iii. Miundombinu ya barabara nyingi ambayo haipo katika njia mbadala za jirani.
iv. Usalama na uzoefu wa Tanzania katika ujenzi wa mabomba yakiwemo Bomba la gesi Asilia kutoka kisiwa cha Songo Songo mpaka Ubungo-Dar, Bomba la gesi asiliakutoka Madimba Mtwara hadi Kinyerezi Dar-es-salaam na Bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanzania hadi Zambia (TAZAMA).
v. Hali ya tambarare katika ardhi ya Tanzania hivyo gharama za utekelezaji kuwa rahisi.
TAMKO LA PAMOJA.
Tamko la Pamoja la kukamilika kwa majadiliano ya vipengele vya mkataba kuhusu utekelezaji wa Mradi husika lilisainiwa tarehe 21 Mei,2017 Jijini Dae-es-Salaam na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri wa Uganda Mhe.Yoweri Kaguta Museveni
KUSAINI MKATABA.
Waziri wa katiba na Shria wa Tanzania Prof. Paramagamba Kabudi pamoja na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni tar 26/05/2017 walisaini mkataba wa INTERGOVERMENTAL AGREEMENT (IGA)-Yaani mkataba wa ushirikiano kati ya Serikaliya Uganda na Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa Ujenzi wa Bomba la kusafirisha
mafuta ghafi (crude oil) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga Tanzania.
UTEKELEZAJI
Mradi huo mkubwa utatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali za Uganda na Tanzania na pia utahusisha kampuni za TOTAL E & P ya Ufaransa, TULLOW OIL ya Uingereza na China National Offshore Oil Corporation (CNOOC) ya China.Makisio ni uwepo wa mapipa Bilioni 1.2 - 1.7 (recoverable).
GHARAMA
Ujenzi wa Bomba hili la mafuta utagharimu jumla ya Dola za Marekani Bilion 3.55 nalitakuwa na urefu wa kilometa 1,445 ambapo litasafirisha mapipa (200,000) na 216,000 kwa siku. kati ya kilometa hizo kilometa 1,149 zitajengwa ndani ya ardhi ya Tanzania.
FAIDA ZA MRADI
i. Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 11,000 za muda mfupi na za kudumu
ii. Kuchochoa utafutaji wa mafuta nchini Tanzania na nchi Jirani hususan katika maeneo linapopita bomba la mafuta.
iii. Kuimarisha matumizi ya Bandari ya Tanga na hivyo kuongeza mapato ya serikali.
NJIA YA BOMBA LA MAFUTA.
Bomba hili litaingia mkoa wa Kagera kutoka Nchini Uganda na kupitia katika mikoa ya Geita,Shinyanga,Tabora ,Singida,Dodoma na Manyara hadi Bandari ya Tanga.
WATUMIAJI WENGINE WA BOMBA
Nchi zinazotarajia kutumia bomba hilo kwa miaka ijayo ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Sudan Kusini,Burundi na pia nchi nyingine za Afrika mashariki.
ENEO ITAKAPOJENGWA GATI
Gati itajengwa nje kidogo ya Mji wa Tanga katika eneo la Chongoleani.
SHUGHULI ZA UTAFITI.
Zoezi la utafiti wa nchi kavu na baharini limefanywa.Tayari sampuli za udongo na maji zimekwishapatikana kwa ajili ya uchunguzi wa takwimu mbalimbali za kihandisi. Maeneo 6 yamekwishachimbwa visima vya sampuli za udongo katika awamu ya kwanza.
Utafiti wa njia nzima ya Bomba unaendelea kwa kuanza kuwashirikisha wadau wote wa Mikoa ambayo bomba litapita.
MIKOA NA WILAYA AMBAYO BOMBA LITAPITA.
MKOA
|
WILAYA
|
KAGERA
|
Missenyi
|
Bukoba Rural
|
|
Muleba
|
|
Biharamulo
|
|
GEITA
|
Geita
|
Chato
|
|
Bukombe
|
|
Mbogwe
|
|
SHINYANGA
|
Kahama Town
|
TABORA
|
Nzega
|
Igunga
|
|
SINGIDA
|
Iramba
|
Mkalama
|
|
Singida Rural
|
|
MANYARA
|
Kiteto
|
Hanang
|
|
DODOMA
|
Kondoa
|
Chemba
|
|
TANGA
|
Kilindi
|
Handeni Town
|
|
Korogwe Rural
|
|
Muheza
|
|
Tanga City
|
Bomba hili linatarajia kukamilika mwaka 2020. Lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli amesisitiza mradi huwo kuweza kuisha hata kabla ya mwaka 2020 kwa kushauri wakandarasi wataojenga Bomba Hilo kufanya kazi mchana na usiku ili kukamilisha mradi huo kwa haraka.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.