Bank ya posta Tanzania TPB imetoa madawati na thamani za walimu kutokana na ombi la uhaba wa shule ya Pongwe jambo linalopelekea kuwa wengi na kusababisha wanafunzi hao kutojifunza vizuri kutokana na mrundikano mkubwa wawapo madarasani .
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Milapwa ameipongeza bank hiyo kwa msaada walioutoa na kuwaomba waendelee kusaidia kwani bado inamahitaji makubwa ambayo bado yanahitajika shuleni hapo
“kwaiyo nyinyi wenyewe mnaweza mkachukua hatua kwa vile mmeshasikia fanyeni hivyo lakini tunawashukuru sana kwa hichi mlicho tusaidia na tunapata moyo sisi kwamba hata tutakapokuwa tunatoa maombi mengine tunasema tunawatu ambao wanatusaidia”amesema Thobias Milapwa
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba Moshingi amesema wanafarijika sana kuwa katika jiji la Tanga na wamesikia changamoto ambazo watu hao wanazo na wakipata chochote hawatasita kuwasaidia
“Tumefarijika sana kuwa hapa katika jiji la tanga na tutajitahidi kukabiliana na changamoto zilizopo lakini pia bank yetu imefarijika sana kuwepo hapa”Amesema Thobias Moshingi
Waziri Kamba ni makamu mkuu wa shule msingi pongwe na Merieni Kanjami ni afisa mtendaji wa kata ya pongwe wameeeleza namna shule hiyo ilivyo na mahitaji makubwa
“uhaba wa vyumba vya madarasa ni 11 ambapo mahitaji halisi ya madarasa ni vyumba 25na vilivyopo ni 14 na kati ya vyumba hivyo vyumba 8 ni vichakavu na vinahitaji ukarabati mkubwa pia shule inahitaji maji kwani yapo maji ya bomba ambayo wanatumia luku na matumizi yanatumia jumla ya shillingi laki nne kwa mwezi gharama ambayo shule inashindwa kuimudu”wamesema Merieni Kanjami naWaziri Kamba
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Ramadhan Possi amesema Halmashauri imetenga kiasi cha shillingi milioni miamoja kwa mwaka wa fedha ikiwa ni makusanyo ya ndani kwaajili ya kuboresha miundombinu ya shule hiyo na kutatua changamoto zote zilizopo.
“Tunatambua shule hii inamahitaji ,mengi kama ilivyosomwa kuna upungufu wa madawati na kama halmashauri tunalitambua kwamba mahitaji hapa ni mengi kwaiyo tunatafuta mbinu itakayo saidia kutatua changamoto hizo”amesema Ramadhan Possi
Elimu ni ufunguo wa maisha kwa hivyo tunapaswa kujitolea kusaidia pale tunapoona kun changamoto zozote katika jamii.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.