Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Ndugu Khalifa Shemahonge ametoa rai kwa walimu ambao watahusika kusimamia mitihani ya darasa la saba inayotarajiwa kuanza siku ya jumatano na kumalizika Alhamisi kusimamia maadili ya kazi kwa kuzingatia taratibu,kanuni na sheria za mitihani ili kupata wataalamu ambao watalijenga taifa .
Mwalimu Shemahonge ameitoa rai hiyo alipokuwa akizungumzia maandalizi ya mitihani ya darasa la saba amesema Halmashauri ya jiji la Tanga ina jumla ya shule 100 ambapo shule 21 Binafsi na za serikali 79 ambazo zitafanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi huku idadi ya wanafunzi ambao wamesajiliwa kufanya mtihani 7401,wasichana 3875 na wavulana ni 3526.
“Mimi nitoe rai kwa walimu watakao simamia mtihani bila shaka wamepewa maelekezo vizuri kikubwa wazingatie taratibu za mitihani lakini pia nidhamu ya kipekee nishauri walimu husika wawe makini kwa sababu wanatengeneza maisha ya watu pamoja na Taifa la kesho hili eneo ni muhimu sana ambalo ni lazima wawe makini “Amesema Afisa Elimu wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Khalifa Shemahonge.
Pia ametoa wito kwa wanafunzi wanaofanya mitihani hiyo kumshirikisha mwenyezi mungu kwa kuomba Dua na Sala mbalimbali kila mtu kwa dini yake kwani mtihani wanaoufanya ni kama mazoezi ya darasani kwani hamna kitu kigumu vyote wamesoma madarasani .
Aidha Shemahonge amepongeza juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Tanga za kuwataka wanafunzi ambao wapo kwenye Madarasa ya mitihani kuwa kwenye makambi jambo ambalo litasaidia kuongeza ufaulu kwa mwaka huu ukilinganisha na miaka ya nyuma .
“Tunatekeleza haya maelezo ya Mkoa au maadhimio ya kikao cha Handeni ,Mwezi wa sita wakati wa likizo wanafunzi wote walisoma ,walikaa kambi na walikula mchana tumekuwa tukifanya tathimini kila wiki katika kipindi cha kambi na hatujaacha mpaka mwisho kuweza kuangalia kwamba matokeo yalibadilika, kwa mapenzi ya mungu tunatarajia matokeo ya mitihani hii yatakuwa mazuri zaidi.”Amesema Afisa Elimu wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Khalifa Shemahonge
Darasa la saba wanatarajia kuanza mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi siku ya Jumatano na Alhamis ya tarehe 11,12 mwezi huu ,hivyo tunapaswa kushirikiana vyema kuwaandaa watoto wetu ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Ndugu Khalifa Shemahonge
akitoa rai kwa wasimamizi wa mitihani ya Darasa la sabaJjijini Tanga.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.