Wakuu wa Idara/Sehemu na Vitengo wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, wamepatiwa mafunzo juu ya mifumo mipya ya kielectronick ya Upimaji utendaji kazi kwa Taasisi (PIPMIS - Public Institutions Performance Management Information System) na Mfumo wa upimaji utendaji kwa wafanyakazi wa umma (PEPMIS - Public Employee Performance Management Information System)
Mafunzo hayo yametolewa leo, Alhamisi Novemba 23, 2023 na Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yanayolenga kutatua changamoto zilizokuwepo kwenye mifumo ya awali ya upimaji watumishi, ambapo mfumo wa PEPMIS utatumika badala ya OPRAS, na PIPMIS umeundwa kutatua changamoto zilizokuwepo kwenye mfumo wa IPCS.
Mfumo huo wa PEPMIS utapunguza na kuondoa matumizi ya karatasi, kuongeza uwazi katika usimamizi wa watumishi na kuondoa upendeleo na uonevu katika upimaji na utendaji kazi kwa watumishi.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.