Mbunge wa Tanga Mjini Mhe.Ummy Mwalimu Leo tarehe 27/4/2021 ametoa madawati 355 yenye thamani ya shilingi milioni 30 ambayo yamenunuliwa kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo.
Mhe Ummy Mwalimu amekabidhi madawati 50 katika Shule ya Msingi Chuda ikiwa ni sehemu ya madawati hayo 355 aliyoyatoa kwa shule nyingine za Msingi Jijini Tanga.
Mhe Ummy ameeleza kuwa akiwa Mbunge wa Tanga ataweka nguvu zaidi katika kutatua kero za Elimu ikiwemo upungufu wa madarasa, madawati na walimu.
Akizungumza baada ya kukabidhi madawati hayo Mhe. Ummy aliwaomba wadau wa maendeleo kusaidia upatikanaji wa madawati ili tumalize tatizo hilo la upungufu wa madawati katika shule zetu na kusisitiza kuwa yeye ataendelea kutumia pesa za mfuko wa Jimbo kutatua uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa.
Kwa upande Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji amemshukuru Mh. Ummy kwa kuchangia madawati hayo kwani yatatatua upungufu uliopo kwa wanafunzi.
Kata zilizofaidika na Mpango huo ni Mzizima, Kiomoni, Chumbageni,Majengo,Marungu ,Msambweni,Ngamiani Kusini,Mzingani na Tongoni.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.