Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba, Septemba 26, 2022 amefika katika kata ya Kiomoni na kuwataka wakazi wa kata za Kiomoni, Mzizima na Mabokweni zilizopo ndani ya Jiji la Tanga, kushirikiana na Serikali katika kutatua mgogoro wa ardhi unaohusu umiliki kati yao, Halmashauri ya Jiji la Tanga na mmiliki wa awali, kampuni ya Amboni Estate.
Mgumba amesema kufika kwake kwa haraka kutatua mgogoro huo, kunatokana na maelekezo aliyopewa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan, ya kuwasikiliza wananchi hao na kuwashauri kwa mujibu wa sheria, pasipo matumizi ya mabavu.
Mgumba anakuwa Mkuu wa Mkoa wa tatu hapa Tanga kuchukua hatua za kumaliza mgogoro wa ardhi katika maeneo ya Amboni na Kange, ambapo wakuu wa Mikoa waliomtangulia, Mhe. Martine Shigella na Mhe. Adam Malima, nao walichukua hatua mbalimbali za kumaliza mgogoro wa ardhi ktk maeneo hayo.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.