Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mhe. Al-Hajj Abdulrahman O. Shiloow amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania (Association of Local Authorities of Tanzania - ALAT) Tawi la Mkoa wa Tanga, katika uchaguzi uliofanyika Jumanne, Mei 23, 2023 kufutia kujiuzulu hivi karibuni kwa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Vijijini, Mhe. Sadick Kallaghe.
Katika mkutano huo wa uchaguzi, ambao wajumbe wake ni Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri ndani ya Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, na Madiwani wawili kutoka kila Halmashauri ndani ya Mkoa, walimchagua Meya Shiloow kwa kura 24 dhidi ya kura 15 alizopata mpinzani wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilindi, Mhe. Idrisa Mgaza.
Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania Bara (ALAT), ni Jumuiya ya Halmashauri zote za Wilaya, Majiji, Manispaa, Miji Midogo na Vijiji, ambayo ilianzishwa mwaka 1984 baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa Serikali za Mitaa kwa Sheria Na. 7 na 8 za mwaka 1982.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.