• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
Tanga City Council
Tanga City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Usafi wa Mazingira
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jiamii na Vijana
      • Maji
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
    • Kata
    • Mitaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Utalii
    • Sekta ya Madini
    • Sekta ya Elimu
    • Sekta ya Viwanda
    • Maeneo ya Nyumba na Makazi
    • Sekta ya Misitu na Mashamba ya Miti
    • Sekta ya Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Usafi na Mazingira
    • Maji
    • Ardhi na Maliasili
    • Ujenzi na Miundombinu
    • Uwezeshaji Wananchi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Siku za Kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Fomu Mbalimbali
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Majarida
    • Taarifa za Miradi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • TangaTV

KAMATI YA USHAURI WILAYA YAJADILI BAJETI YA BILLION 72.1

Imewekwa: March 2nd, 2023

Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC), leo Jumatatu, Februari 27, 2023, imepokea wasilisho la rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa mwaka wa fedha 2023/2024, yenye makisio ya makusanyo na matumizi ya shillingi Billion 72,111,627,000.00 kwa lengo la kushauri maeneo ya kipaumbele katika utekelezaji wake.


Akifungua kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hashim Mgandilwa amewataka wajumbe kufikiri na kutoa ushauri kwa Halmashauri namna ya kuboresha ukusanyaji wa mapato kwa kuibua vyanzo vipya vya mapato, na kuwekeza katika miradi itakayozalisha mapato endelevu.


"Sisi kwa umoja wetu ndio wenye wajibu wa kutoa mipango, kwa kuangalia tunahitaji Tanga ya namna gani. Tupitie mapendekezo ya bajeti waliyotuletea na tuweze kupendekeza yale tunayofikiri yatakwenda kuijenga Tanga tunayoitaka." Amesisitiza Mgandilwa


Awali, akiwasilisha Mpango na Bajeti ya Halmashauri kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Mkuu wa Sehemu ya Mipango na Ufuatiliaji Bw. Simeon Vedastus amesema kati ya shillingi Billion 72.1 zitakazo kusanywa, Billion 19.1 ni mapato ya ndani, ambapo asilimia 70 ya fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi ya maendeleo.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt. Sipora Liana amesema Jiji limetekeleza miradi mingi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa 100 kwa shillingi Billion 2, huku akiwataka Watendaji wa Kata kuhamasisha wana vikundi vya kiuchumi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu kujitokeza kuomba mkopo wa kuanzisha viwanda vidogo kwani fedha zipo kuwezesha makundi hayo.


Akijibu baadhi ya hoja za wajumbe, Mstahiki Meya Al-Hajj Abdulrahman Shiloow amesema Halmashauri tayari inaendesha shule mbili za mchepuo wa kiingereza, na inakusudia kujenga shule zingine mbili, moja ikiwa Maweni njia ya Korogwe, na nyingine itajengwa njia ya Pangani.


Kikao hiki ni muendelezo wa vikao vya kupitia rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri kabla ya kuwasilishwa katika Mkutano maalum wa Bajeti wa Baraza la Madiwani.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ. March 09, 2025
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA JIJI TANGA September 27, 2024
  • TAARIFA YA MSIBA September 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 26, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TANGA: MABORESHO DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA FEB. 13, 2025

    February 04, 2025
  • MENEJIMENTI WAPONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI, UMALIZIAJI WA VIPORO.

    February 04, 2025
  • AFUA ZA LISHE ZAFANYA VIZURI TANGA JIJI

    January 24, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAKAGUA MIRADI.

    January 16, 2025
  • Angalia Zote

Video

Baraza la Madiwani la kwanza 2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matumizi ya TEHAMA kwa Jiji la Tanga
  • Kata na Mitaa ya Jiji la Tanga
  • Manual ya mfumo wa FFARS
  • Muongozo wa ugawaji wa kitambulisho cha mjasiliamali
  • Jarida la Mifumo Yetu - Novemba 2018-Januari 2019
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Tangazo kuhusu watumishi waliomba vibali vya uhamisho
  • Kuanza Ujenzi na Kupata Kibali cha Ujenzi
  • Kuhusu kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi

Tovuti Linganifu

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Mfumo wa Kuomba Vibali vya Nje ya Nchi
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Independent Avenue

    Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga

    Simu ya Mezani: 027 2643068

    Simu ya Mkononi:

    Baruapepe: info@tangacc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.